Huku ongezeko la visa vya malaria vikitarajiwa kuongezeka kutokana na mvua ya masika inayonyesha kila uchao,serikali imeanzisha kampeini dhidi ya malaria na kutoka wiki ijayo itaanzisha operesheni ya kunyunyuzia dawa zaidi ya nyumba milioni moja katika mikoa ambayo huathiriwa zaidi na malaria. watoto tisini na sita hufa kila siku humu nchini na serikali inanuia kupunguza visa hivi kwa asilimia 40% kupitia operesheni hiyo.