Serikali imepata pigo kuhusiana na ombi lake kuitaka mahakama ya rufaa isimamishe kwa muda agizo la kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar Al- Bashir endapo atazuru kenya. Hii ni baada ya mahakama ya rufaa kupinga ombi la mwanasheria mkuu githu muigai kutaka agizo la kumkamata bashir lisimamishwe kwa muda hadi pale rufaa aliyowasilisha mahakamani itakaposikizwa.majaji watatu wa mahakama ya rufaa hata hivyo wameamua kwamba sababu alizotoa mwanasheria mkuu hazikutosha kusimamisha agizo lililotolewa na jaji nicholas ombija wa mahakama kuu.


Court rules on Al-Bashir