Baada ya kutangazwa kuwa uchumi umekuwa kwa asilimia 2.6, sasa imeibuka kuwa sekta ambazo zingekuza uchumi zaidi ziliathiriwa mwaka jana kutokana na changamoto zilizokabiliwa kama hali ya ukame na matatizo ya kifedha ulimwengu mzima. Lakini ikikumbukwa kuwa sekta kama ya kilimo inachangia sana katika kupiga jeki uchumi wa nchi yoyote barani Afrika, wadadisi wanasema itakuwa jambo la kufana iwapo serikali itamudu mbinu za kuboresha ukulima na sekta zinazochangia kukuza uchumi wa Kenya.