Na, Hassan Ali
Kivumbi kinatarajiwa leo hii katika mbio za mchujo mita 800 kinadada kuanzia saa kumi na moja kasoro dakika tano. Wakenya watakuwa wakiwakilishwa na Eunice Sum, bingwa wa dunia mwaka 2013, bingwa wa riadha chipukizi mwaka 2014 Margaret Nyairera na bingwa wa fedha mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika Winy Chebet. Badaye saa kumi na moja na dakika tato, kutaandaliwa mbio za wanaume kusaka tiketi ya fainali wanaume mita alfu tano. Bendera ya kenya itakuwa ikipeperushwa na bingwa wa dunia medali ya fedha Caleb Ndiku akisaidiwa na Isaiah Kipalagat na Charles Yosei. Kikwazo hapa kwa Wakenya kutwaa medali ya dhahabu ni Mwingereza Mo Farah, ambaye Jumamosi alitwaa medali katika mbio za mita 10k.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.