Uwezo wa Vijana Katika Maandamano ya Demokrasia
Published Jun. 28, 2024
00:00
00:00

Vijana wa Gen Zs na vijana wengine ambao wamekuwa wakiendeleza maandamano dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 wametukumbusha uwezo tulio nao kama wananchi wapigakura. Uwezo wa kupiga kura kuwachagua viongozi wetu, lakini zaidi kuwawajibisha wanapokuwa ofisini. Harakati hii haifai kukoma. Huu unafaa kuwa mwanzo tu wa kutetea Katiba yetu na kudai uongozi bora ambao tunastahili.