Serikali Yalazimika Kukubali Ukweli wa Maandamano ya Vijana
Published Jun. 24, 2024
00:00
00:00

Serikali sasa imegundua kuwa haiwezekani kupuuza maandamano yanayoendelezwa na kizazi cha vijana dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024. Rais mwenyewe amekiri kuwa ipo haja ya kufanyika mazungumzo kati yake na vijana hawa. Kiukweli, hakuwa na budi. Kuanzia mwanzo haingewezekana tu kuwapuuza vijana hawa kutokana na sababu kadhaa.