Cheche baina ya timu za ‘Embrace’ na Inua Mama

Ulingo wa kisiasa nchini Kenya haujawapa wanawake kwa jumla nafasi ya kumenyana na wanaume.

Tangu Kenya ipate Uhuru, kuchaguliwa kwa mwanamke katika nyadhifa mbali mbali za kisiasa kumeonekana kama ndoto machoni mwa wengi wanaoamini kwamba nafasi ya mwanamke katika jamii ni mekoni na wala si uongozini.

Kufuatia marekebisho ya katiba na kupanuka kwa nafasi za elimu kwa wanawake kupitia technolojia na utandawazi, utamaduni wa kigeni unmepanua mawazo ya wanawake ambao wameonekana kuchukua usukani kwa kishindo kutetea masilahi yao na yale ya vijana hususan mtoto wa kike ambaye amedhalilishwa kwa miaka na mikaka kutokana na mila ya Kiafrika.

Katiba ya mwaka 2010 imetoa nafasi kwa wanawake kujiunga na siasa kupitia kuchaguliwa moja kwa moja kupiutia nafasi za waakilishi wa kike katika Kaaunti na uteuzi maalum uliotengewa vyama baada ya kila uchaguzi mkuu.

Mdahalo kufanyia marekebisho katika ya waka 2010 ili kubuni nafasi ya waziri mkuu na manaibu wawili ambao umeletwa na mpango mzima wa kujenga madaraja ya uhusiano mwema umeleta mgawanyiko miongoni mwa wanasiawa wanawake.

Makundi ibuka ya “Embrace” yaani “Kumbatia Umoja wa Kitaifa chini ya Uongozi wa Katibu msimamizi katika Wizara ya Vijana, Rechael Shebesh na lile la Inua Mama-Jenga Nchi linaloaminika kudhaminiwa na Naibu wa Rais Dkt. William Ruto chini ya uongozi wa Mbunge wa Kandara Alice Wahome yanaonekana kuvuta pande mbili tofauti huku kundi la Embrace likiunga mkono marekebisho la ya katiba na Inua mama li kubuni nyadhifa Zaidi za uongizi na lile la inua mama lilipiganisha kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida kama njia moja ya kumpigia debe naibu Rais Dr. William Ruto.

Wakati Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa upinzani, aliyekuwa Waziri Mkuu Raila odinga walipokutana kwa tukio la kipekee la “Handisheki” walijadili maswala tata yanayolikabili taifa na kukubaliana kubuni jopo la pamoja kutathmini mapendekezo yao hapo ndipo mpango wa kujenga madaraja ya uhusiano mwema maarufu BBI ulibuniwa.  

Kikosi cha “Embrace” kimefanya mikutano maeneo ya Pwani, Bonde la Ufa na Kaskazini Mashariki mwa nchi huku sauti kuu ikiwa marekebisho ya katiba kama njia ya kumaliza uhasama ubnaoweza kusababisha machafuko baina ya washindani wa kisiasa.

Kundi la Embrace linaonekana kuwakashifu wenzao wa Inua Mama-Jenga nchi kama njia ya kujipatia umaarufu nacho kikosi cha Inua mama, kikitilia shaka uhalisi wa wenzao wa mrengo wa Embrace.

Kwa wakati mmoja mbunge wa Malindi Aisha Jumwa na Seneta wa Nakuru Susan Kihika waliwakashifu vikali wafuasi wa kundi la Embrace kwa kutumiwa na vigogo wao wa kisiasa kuzima azma ya Naibu wa Rais Dkt. William Ruto ya kupigania uongozi wa nchi mwaka 2022 ilihali wanajifi cha chini ya kivuli cha kuwaunganisha Wakenya.

Kikosi cha Inua Mama-Jenga Taifa kimekuwa kikiyatunuku makundi ya kina mama na vijana mashinani vifaa vya kufanyia Biashara kama vile Pikipiki maarufu Boda Boda, meko za gesi ya kupikia, ngombe wa maziwa, kuku wa mayai na tinga tinga za kulima mashamba ili kutumia nafasi hiyo kunadi sera za Naibu wa Rais, jambo ambalo halijawafurahisha wapinzani wanao wanaotilia shaka chanzo cha mamilioni ya hela wanazotoa kwenye mikutano ya hadhara kila wikendi.

Vikosi vyote viwili vimekuwa vikirushiana cheche za maneno si haba huku kundli la Inua Mama-Jenga Taifa likiwasuta wana “Embrace” kwa kuwahutubia wananchi mchana kutwa kwenye jua kali na kuwaacha waondoke kuelekea manyumbani mikono mitupu bila kujali jinsi ya kuimarisha hali yao ya maisha.

Aidha hatua ya mirengo hii ya kinamama na harakati za kuwapigia debe wagombea mbali mbali wa viti vya uchaguzi wa mwaka 2022 inadhihirisha wazi kwamba demokrasia imekomaa nchini Kenya.

Nafasi ya kisiasa kwa wanawake zimeonekana kuimarika ikilinganishwa na awali ambapo wabunge wanawake hawangeweza kujibu malumbano makalli kutoka kwa wenzao wa kiume jukwaani bila uoga kama ilivyoshuhudiwa kwenye mkutano wa Voi hivi majuzi ambapo kundli la Inua Mama-Jenga Taifa liliitishia kuwasilisha ombi la kumtimua Mbunge mteule Maina kamanda kutoka chama cha Jubilee kwa kutangaza kumuunga mkono mgombea wa chama cha ODM kwenye uchaguzi mdogo ujao wa Kibra.

Licha ya makundi ya Embrace na Inua Mama-Jenga Taifa kuonekana kunoa makali yao kukabiliana na upinzani katika safari yao ya kufanikisha malengo yao, wapo wanaodhani kwamba kina mama hao wanatumiwa na wenzao wa kiume kupitisha ujumbe na kutekeleza matakwa yao na wala sio ndoto ya wanawake wote kote nchini.

Timu ya “Embrace” inawajumulisha wabunge wa kike kutoka vyama mbali mbali vya kisiasa magavana na baadhi ya makatibu wasimamizi miongoni mwao Katibu Recho Shebesh, wabunge Gladys Wanga, Millie Odhiambo, Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi Waiguru na Charity ngilu wa Kitui.

 Kwa upande wa vuguvugu la Inua Mama-Jenga Taifa wafuasi ni wabunge wa kike kutoka vyama vya Jubilee na ODM miongoni mwao Gladys Sholei, Susan Kihika, Alice wahome, Aisha Jumwa na mbunge mteule Falhadha Iman miongoni mwa wengine.