Mgombea urais wa UDA, William Ruto amezindua manifesto yake akiangazia nguzo sita; kupunguza gharama ya maisha, kumaliza uhaba wa walimu, matibabu bila malipo, kujenga nyumba elfu 250 kila mwaka, kukuza biashara na kuimarisha kilimo. Ahadi hizi zinatekeleka? Upande mwingine Wajackoyah ameweka wazi manifesto yake akijumuisha mambo ya kiajabu. Mara atahamisha jiji la Nairobi hadi Isiolo, sijui kufuga nyoka, kuvunja sekta ya bodaboda na kuwaajiri wahudumu hao katika mashamba ya bangi na mengine mengi ya kushangaza. Ni manifesto gani ni nzuri? Halafu Kenya Kwanza inasema bandari ya Mombasa imeuzwa huku serikali ikikana. Kadhalika Baba ameanza vita dhidi ya Chebukati. Anasema manual register sharti itumike sambamba na electronic. Chebukati anasema la hasha. Kwa nini Baba anasisitiza ni lazima manual itumike? Haya yanajiri huku suala la zoning likitikisa nyumba ya Baba. Wagombea wasio maarufu wanaambiwa wajiondoe kuwapisha wenye nguvu. Benard Lusigi wa Kakamega, Edwin Mbugua wa Nyeri na Martin Ndiema akiwa Trans Nzoia wanatupambia makala haya.