Familia ya ajuza mmoja katika Kijiji Cha Nzoia Mukhuyu Kaunti ya Kakamega inalilia haki baada ya ajuza huyo mwenye umri wa miaka tisini na minane kuvamiwa usiku wa manane na kubakw

Familia ya ajuza mmoja katika Kijiji Cha Nzoia Mukhuyu Kaunti ya Kakamega inalilia haki baada ya ajuza huyo mwenye umri wa miaka tisini na minane kuvamiwa usiku wa manane na kubakwa.

Ajuza huyo amesema kuwa mshukiwa George Bushasha aliingia chumbani anakolala  na kutekeleza unyama huo na baadaye kumshambulia kwa kumpiga kabla ya kutoweka.

Familia ya ajuza huyo sasa inadai kutishiwa na mshukiwa ambaye licha ya tukio hilo kuripotiwa kwa polisi katika Kituo cha matunda bado hajakamatwa.