Mabaki zaidi ya ndege yapatikana Nakuru

Na, Sarah otieno
Mabaki zaidi ya ndege yapatikana Nakuru
Mabaki zaidi ya ndege iliyoanguka katika Ziwa Nakuru na kusababisha vifo vya abiria watano, yamepatikana pamoja na nguo zinazoshukiwa kuwa za waliokuwa katika ndege hiyo.
Mabaki hayo yamegunduliwa na wapigambizi ambao wamekuwa wakiendesha shughuli za kusaka mili iliyosalia. Kufikia sasa ni mili mitatu pekee iliyopatikana miongoni mwa mitano, ukiwa takriban mwezi mmoja sasa tangu ndege hiyo ianguke.
Siku ya Ijumaa wiki iliyopita, mwili wa Veronica Muthoni ambaye alikuwa mmoja wa abiria katika ndege hiyo ulipatikana. Mili mingine ambayo tayari ilipatikana na kuzikwa ni ya aliyekuwa rubani, Apollo Malowa na Anthony Kipyegon. Mili ambayo haijapatikana ni ya Sam Gitau na John Mapozi.

Related Topics