Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Christ Is The Answer Ministry, CITAM, David Oginde ndiye Mwenyekiti mpya wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC.
Oginde anachukua nafasi ya Eliud Wabukhala aliyestaafu baada ya kukamilisha muhula wake katika EACC.
Kuidhinishwa kwa Oginde kunajiri baada ya wabunge kujadili ripoti ya Kamati ya Haki na Sheria-JLAC, ambapo wameidhinisha wakimtaja Oginde kuwa mchapakazi. Pia wamemtaka kuhakikisha suala la ufisadi linakabiliwa vilivyo. George Murugara ni Mbunge wa Tharaka.