Mwili wa mwanamme mmoja umepatikana mapema leo hii katika eneo la Nkaimurunya, Kaunti ya Kajiado.
Polisi wanasema mwili huo umepatikana ukiwa na majeraha mabaya ya visu kifuani, shingoni na mgongoni.
Uchunguzi umeanzishwa mwili wake ukipelekwa katika Hifadhi ya City.