×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Utafiti: Viazi vitamu vyasaidia macho

Health & Science

 

Kulingana na shirika la Ugunja Community Resouce Centre, viazi tamu viko na madini aina ya Vitamini A ambayo ni muhimu kwa kusaidia machoya mwanadamu. Mtu anayekula viazi tamu hasa

vile vya rangi ya machungwa sio rahisi awe na matatizo ya macho maishani. Viazi hivi tamu ni miongoni mwa vyakula vinavyopendwa zaidi na baadhiya jamii za Kenya. Viazi huwa na ladha tamu ya sukari ndio sababu watu wanapenda sana kula ingawaje ni wachache ndio wanafahamu jinsi ya kuandaa. Kuna aina nyingi ya vyakula au vitafunio ambavyo vimetengenezwa kwa Nkutumia viazi tamu. Miongoni mwa vyakula hivyo ni crackies, crisps, mandazi, keki, minsed,unga wa uji na ugali, dried chips, chapati.

 Vyakula hivi vyote vinaweza kuundwa kwa kutumia viazi tamu na walehawajui hushangaa sana. Watu wamekuwa wakijuwa kwamba viazi tamu huchemshwa tu na kuliwa,vyakula vyengine vinavyotokana na viazi tamu hawajui kabisa. Hivyo basi, kuna haja ya watu kufunzwa kujua mbinu nyingi za kuandaaau kupika viazi tamu, wengi huchemsha tu. Viazi tamu maganda yake ukiyakausha na kusaga ni chakula cha mifugokama vile kuku na nguruwe. Afisa wa shirika la Ugunja Community Resource Centre, anasema kwamba kuku anayekula maganda ya viazi tamu hutaga mayai mengi na nguruwe hunenepa sana

Related Topics


.

Popular this week