Na, Suleiman Yeri
Eneo la Kisii lina uwezo wa kuamua ni nani atakayeshinda kinyang'anyiro cha urais wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Ndiyo kauli ya Mbunge wa Kitutu Chache, Richard Onyonka kufuatia hatua ya baadhi ya viongozi wa eneo hilo kukutana Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake katika, Ikulu ya Nairobi. Onyonka amesema jamii ya Kisii ni kubwa na imesambaa kila sehemu nchini na kwamba wako tayari kumuunga mkono mgombea wa urais ambaye wana imani kwamba ataibuka mshindi na kuliendeleza eneo hilo. Seneta wa Kisii, Chris Obure kwa upande wake anasema ziara hiyo ya Ikulu haimaanishi kuwa wanapanga kuhamia muungano wa Jubilee. Kwa mujibu wa Obure, lengo kuu la ziara hiyo ni kuhakikisha kuwa eneo hilo haliachwi nyuma kimaendeleo na kupuuza madai ya baadhi ya viongozi kwamba ililenga kuwanufaisha wachache.