Na Mate Tongola

MIONGONI mwa Tume kumi na tano zinazohudumu nchini, ile ya Huduma za Mahakama, JSC ndiyo inayoongoza katika kutozingatia mchanganyiko wa watu wa makabila mbalimbali katika uajiri.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa, NCIC, JSC inakiuka kifungu cha saba ibara ya pili ya sheria za NCIC kwa kuwaajiri zaidi ya watu thuluthi  ya wafanyakazi kutoka kabila moja.

Ripoti hiyo imefichua kuwa asilimia 39.1 ya wafanyakazi wa JSC ni wa jamii ya Kikuyu, hii ikiwa asilimia sita zaidi ya kiwango kinachostahili, kwa mujibu wa sheria za NCIC.

Aidha, ripoti hiyo imebainisha kuwa usajili kwenye kaunti umeendelea kukiuka sheria huku kaunti kumi na tano miongoni mwa arubaini na saba zikitoa asilimia thelathini ya kazi kwa watu wa jamii ambazo hazipatikani kwenye maeneo hayo.     

 


JSC;NCIC