Idadi ya watu waliofariki kufuatia mkasa wa moto uliotokea katika kituo kimoja cha gesi mjini nyeri imeongezeka na kufikia watu wanne. Watu hao wawili waliofariki ni miongoni mwa wale waliosafirishwa na kuletwa kwa matibabu maalum katika hospitali kuu ya kenyatta hapa jijini nairobi. Uchunguzi sasa umeanzishwa kubaini chanzo cha moto huo