Je, masaibu ya Seneta Wetang’ula ndiyo yamkumba Matiang’i?

Loading Article...

For the best experience, please enable JavaScript in your browser settings.

Kiongozi wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoun na Seneta wa Bungoma Moses Wetang'ula. [Photo: Pambazuko]

Lawama la vidole vya lawama kuoteshwa kwa walengwa wa sakata la dhahabu ghushi na ulanguaji wa mamilioni ya pesa kutoka kwa gwiji mmiliki wa hekalu za matajiri wa ghuba la uajemi, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoun zaonekana kutanda pembe zote za Kenya.

 Baada ya kuwaalika viongozi wa kitaifa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga mnamo tarehe 27 mwezi Aprili mwaka huu katika maeneo yake ya Dubai, Sheikh amepata sauti zaidi na sasa anataka jambo moja tu litimizwe; Pesa zake ama dhahabu kama kweli ingalipo ama ni marimbembe ya sampuli gushi! Hata kabla ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuzuru Dubai pamoja na Rais Uhuru, yeye mapema ya Aprili aliwahi ku? ka kuelezewa zaidi kabla ya kurejea na kumpatia uhondo kamili rais kuhusiana na sakata hiyo na mlalamishi gwiji huyo.

Sasa basi kabla ya gazeti la The Standard kubwagiza uhondo kamili kuhusiana na sakata hii ama kashfa mnamo Mei 13, tayari viongozi hawa wawili walikuwa wamekwisha upata ukweli fulani kuhusiana na jambo zima hili.

Siasa kando

Kwa kawaida ya jambo zito kama hili, hudakiwa na wanasiasa wa mirengo tofauti wakati linapozuka na hata mwishowe kuharibu ama kulegeza ushahidi kwa malengo fulani. Kama kiongozi wa nchi na baba wa taifa, bila shaka Rais Uhuru aliagiza idara husika kuchunguza mara moja sakata hii na kujitokeza kwamba baadhi ya viongozi wa kuheshimika pia wamo msururuni huo. Kinara wa Ford Kenya Moses Masika Wetangula ndiye wa kwanza ambaye tangu kuchipuka kwa kashfa hii, kamwe hapati usingizi wala kula kama kawaida yake.

Amezingirwa aidha kwa kutajwa moja kwa moja kupitia kwa unakiliaji wa mazungumzo ya simu ambayo yadaiwa kuwa yake na gwiji huyo wa Dubai au hata kudhaniwa kwamba alihusika kwa njia moja au nyingine kuhusiana na biashara hii ghushi. Kama kiongozi, huenda akawa alihusishwa kama wakili ama kinara mwenye ura? ki mpana unaojumuisha wanasiasa, ulinzi ama usalama, idara ya mahakama na kadhalika kwamba anasaidia kwa vyovyote vile endapo kutachipuka kama ilivyochipuka.

 Safari hii imekuwa mbaya zaidi kwani jambo linapogusa viongozi wa nchi kama vile Sheikh na Uhuru mezani, basin yang’arika huenda wakaona cha mtema kuni. Ku? kia sasa, mkuu wa mashtaka Noordin Hajj anasubiri kuchunguzwa kwa mazungumzo ya simu yaliyonakiliwa na kusambazwa kote mitandaoni kujua mbivu na mbichi kabla ya kumwezesha kumpatia nguvu ya kumhoji seneta wa Bungoma na wenzake atakaowataja kutoa mwangaza wa ukweli wa mambo.

Huku watu wengi wakimlenga seneta Moses Wetangula kuhusiana na suala hili, wanasiasa wengine wameanza kutumia fursa hiii kuchunguza ni idara gani ama ipi ya serikali ililegeza kamba zake ili kuanza kuishambulia kwa kuho?a kwamba huenda ilishirikishwa kwa njia moja ama nyingine. Idara ya kwanza ama wizara ya mwanzo kumwilikwa ni ya Waziri Fred Matiang’i ambapo wanasiasa fulani wameanza kumweka kwenye laini moja na seneta Moses Wetangula kumsulubisha kwa sakata hii.

 Shauku ya ODM

Shauku la kwanza lajichomoza na mrengo wa chama cha ODM ambacho badala ya kumtetea kinara mwenza wa kumfurusha a? sini ilhali haijajitokeza kimasomaso kwamba alihusika moja kuwa moja na sakata ya dhahabu kama inavyosemwa na wanasiasa wengine.

Kupitia kwa taarifa yake kwa vyombo vya habari, mwenyekiti wa kitaifa wa ODM, John Mbadi ameelezea kinaga ubaga kwamba kambi ya wanasiasa ya naibu wa Rais William Ruto ni kana kwamba wameanzisha sokomoko la kumsingizia waziri wa uslama wa ndani kuwa mmoja wa waliohusika kwenye sakata ya dhahabu ndio wawe na nguvu ya kumn’goa mamlakani.

 “Niko na ripoti kamaili kwamba kunao wabunge wawili wameamrishwa kutengeneza hoja bungeni kuleta mswada dhidi ya Waziri Matiang’i. Twajua mipango yao lakini wafahamu kwamba tutakabiliana nao bungeni kadiri watakavyokuja” anakiliwa mwenyekiti wa ODM. Maswali ambayo yanazidi kumiminika kutoka kwa Wakenya, ni jinsi suala hili litakavyothibitiwa kwani yasemekana kulingana na gwiji huyo wa Dubai hataki kujua ila anataka pesa zake ama dhahabu ambayo sote tunauhakika kwambahakuna.

Hatujui Moses Wetangula na wenzake wakishindwa kumlipa Sheikh atatufukuzia dada zetu na kaka zetu wanaojitafutia riziki Dubai ama atawatumia mamluki kuja kutudhuru kwa kuwa haki ya mtu haizami. Wengi wanasikitika hususan Wakenya wanaoishi mwambao wa pwani ambao wangali na kumbukumbu za picha za mababu zao wakati wakifungashwa na Warabu kama watumwa.

Adhabu ambayo washukiwa wa sakata hii wanaweza kupatiwa kule Uarabuni, haifai hata kutabirika kwani huwa ni uchungu zaidi ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Kulipiwa deni pia sioni kama inawezekana lakini kwa seneta Moses Wetangula ambaye twamuonea huruma zaidi kwa kutajwa moja kwa moja, tungemrai amlipe Sheikh aidha kwa kusaidiana na wenzake wahusika ama kwa kunadi mali yake, kwa kiongozi wa chama kama yeye, milioni 400 haimchanganyi kamwe.