Boko Haram na donda la ugaidi Nigeria kaskazini

Loading Article...

For the best experience, please enable JavaScript in your browser settings.

Jopo la Boko Haram kusababisha maafa nchini Nigeria kaskazini kila kukicha ni jambo la kusikitisha sana. Kufaulu kwa Rais Muhammadu Buhari kwenye uchaguzi Nigeria kunatoa matarajio mapya ya kupata suluhu kwa jambo hili lililokumba nchi nzima ya Nigeria.

Linaloshangaza ni kwamba kikundi kidogo cha magaidi kama Boko Haram linaweza kusababisha maafa vile wamefanya eneo za Borno na Maiduguri. Ukinoa bongo, inaonekana bayana kwamba kunao maafisa kwenye idara za kiusalama Nigeria wanaounga mkono wanamgambo wa Boko Haram.

Jumuia ya kimataifa yakiwemo Chad, Niger na Cameroon zimetia motisha juhudi za Nigeria kuangamiza Boko Haram. Uongozi wa Bwana Buhari utapata pigo kubwa asipoweza kutatua bughdha inayosababishwa na Boko Haram. Serikali ya Bwana Jonathan ilifeili kwenye uchaguzi kwa kutowajibika kukumbana na matatizo ya Nigeria hususan janga la Boko Haram.

Itabidi Bwana Buhari anoe bongo na kuongeza maarifa jitihada zote za kidiplomasia, kijeshi na kikatiba kumaliza donda ndugu la Boko Haram kaskazini mwa Nigeria.