×

SENSA: Jamii za Agikuyu na Abaluhya zaongoza kwa idadi ya Wakenya nchini huku Kuku wakiwa wanyama wengi nchini.

Awamu ya nne ya ripoti ya ya watu iliyofanywa mwezi Agosti mwaka jana imeonyesha kuwa iadai ya wanawake imeshinda ya wanaume kwa 466,660. Idadi lkamili ya Wakenya ni milioni47, 564, 296, wanawake wakiwa 37,724,850 na wanaume ni 24,041,716. Huku watu wenye jinsia isiyokuwa bainifu, intersex wakiwa 1,524.

Vilevile wanawake, wanaongoza kwa idadi ya Wakenya walio na Ulemavu. Idadi kamili ya Wakenya wenye ulemavu ni 918, 270, huku wenye ulemavu wa ngozi wakiwa 9,728.

Jamii ya Agikiyu ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu nchini Kenya kwa kufikisha milioni 8.14, huku jamii ya Dahalo ikiwa na idadi ya chini kabisa ambapo ni watu 575.

Ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Takwimu KNBS Zachary Mwangi, akisoma ripoti ya sensa ya watu iliyofanywa mwezi Agosti mwaka jana.

Jamii ya Abaluhyia inafuata kwa milioni 6. 82, Kalenjin milioni 6. 3, Waluo milioni 5. 1, Kamba milioni 4.6, Jamii ya Somali iliyoko Kenya ikiwa miloni 2.7, Kisii milioni 2.7, mijikenda milioni 2.4, Ameru milioni 1.9 na Maa milioni 1.2.

Vilevile ripoti hiyo imeonesha kuwa miongoni mwa miji mikuu jiji la Nairobi linaongoza kwa idadi ya watu milioni 4.3, Mombasa milioni 1.2, Nakuru 590,674,  Eldoret  475, 716.

Upande wa dini Wakristu ni wengi kwa asilimia 85. 5 ambapo ni milioni 33. 4 huku Waislamu wakiwa asilimia 11. Miongoni wa Wakristo, Waprotestanti wanaongoza kwa asilimia 33. 4, Wakatoliki asilimia 20. 6 na Waevanjelisti wakiwa asilimia 20.4.

Upande wa kilimo, ukulima wa mimea unaongoza kwa asilimia 87.4 , mifugo asilimia 74.4 huku kuku wakiongoza kwa idadi ya mifugo kwa milioni38.8,  mbuzi milioni 28, Kondoo milioni 19, Ng'ombe milioni 15.8.

Ripoti hio imeonyesha kuwa Wakenya wenye ulemavu walio na umri wa miaka 5  na zaidi ni 918, 270, wanawake wakiongoza .Idadi ya Walio na ulemavu wa ngozi ikiwa 9,728.

Upande wa teknolojia Wakenya milioni 20.4 salio zaidi ya 3 wanamiliki simu za mkono

Idadi ya waliojiunga na vyuo vikuu imeongezeka kutoka 171,855 mwaka 2009 hadi 470,983 mwaka 2019. Vilevile idadi ya waliojiungana vyuo vya kiufundi imeongezeka kutoka 325,196 mwaka 2009 hadi 506, 109 mwaka 2019.

Related Topics