Please enable JavaScript to read this content.
Maombi kwa wanasiasa
yana maana gani
hasa mnapozunguka kwa makanisa
msitilie maombi mzaha
leo mtakua Afraha
mkisheherekea kwa furaha
mashtaka mepita ni raha
msitilie maombi mzaha
vilio vya wahasiriwa hakika
mbinguni vimeskizwa
karibuni nao watajibiwa
msitilie maombi mzaha
Stay informed. Subscribe to our newsletter
wakati wa ghasia mlinyamaza
Ocampo alipofika mlikaza
kwa shida maombi yawaliwaza
msitilie maombi mzaha
sasa mwajidai washindi
meshamiri taarifa na vipindi
maombi meandaa kwa vikundi
msitilie maombi mzaha
unyenyekevu ndio mwanzo wa baraka
tena chanzo cha ushindi
kwenu,kielelezo
msitilie maombi mzaha
mwafaa kuomba msamaha
kwa wale mlowakosesha raha
wakati wa kampeni,ushindi furaha
msitilie maombi mzaha
maombi yawe ya amani
utangamano na uridhiano nchini
serikali,wananchi na upinzani
msitilie maombi mzaha