23rd May, 2021
Inajulikana kama ugonjwa wa aibu. Wanawake wengi wanaogua Fistula hujitenga kutoka kwa wakati, na mara nyingi hukumbwa na msongo wa mawazo kutokana na ugonjwa huo. Dunia inapoadhimisha siku ya kudhibiti ugonjwa wa Fistula, ufahamu kuhusu ugonjwa huu utasaidia kuhamasisha wanawake haswa walio mashinani kutafuta huduma za afya kwa sasa kenya inakumbwa na uhaba wa madaktari wa upasuaji wa Fistula, huku visa vingi vya fistula vikikosa kupata suluhu. Fistula ni ugonjwa ambao husababisha shimo kubwa kati ya njia ya uzazi na njia ya mkojo unatokana na mama kuwa na uchungu wa muda mrefu bila matibabu.