20th June, 2020
Ni wiki sasa baada ya ghasia kushuhudiwa kwenye mazishi ya msanii wa ohangla Abenny Chachiga, ambapo idara ya polisi katika kituo cha Central Mjini Kisumu wakiongozwa na OCPD Peter Katam, waliitembelea familia ya marehemu na kuifariji. Abenny alizikwa wiki jana mwendo wa saa nane za usiku katika mazishi yaliogubikwa na ghasia kati ya polisi na wenyeji waliotaka wapewe mda zaidi kumuomboleza. Maafisa wa polisi waliwasili kwenye magari yao na kuelekea moja kwa moja hadi katika kaburi lake na kutoa heshima zao za mwisho baadae kupeana misaada ya vyakula na barakoa kwa familia hio. Wakizungumza na wanahabari, katam alisema familia imempoteza msanii mwenye talanta na msimamizi wa familia aliyewavutia vijana. Pia waliiomba radhi familia hio kutokana na ghasi zilizozuka. Mamake marehemu aliwashukuru maafisa hao huku akiitisha usaidizi zaidi kutoka kwa wahisani.