×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Nyakeyo kuchoma nyumba mbili za mshukiwa wa urogi

10th July, 2018

Wakazi wa kijiji cha Gekongo huko Nyakeyo Kaunti ya kisii wamepigwa na butwaa baada ya wanafunzi wa Shule ya Upili ya Nyakeyo kuchoma nyumba mbili za familia moja wanayodai wamemroga mwanafunzi mwenzao ambaye alifariki juma liliopita baada ya kuugua kwa mda.

Wanafunzi hao waliokua na ghadhabu waliwasili shuleni mwao jumatatu, kuomba kwenda kuwapa pole familia ya muathiriwa, na walipofika na kujuzwa kuhusu madai ya urogi, walichukua hatua hio mikononi mwao.

Mwanafunzi mmoja ambaye hakutaka kutambuliwa, alikiri kuichoma nyumba ya shemeji ya muathiriwa anayeaminika kumroga na hatimae kufariki. Kisha walifululiza hadi nyumbani kwa baba ya msichana anayedaiwa kumroga na kuichoma nyumba yake pia, kwa madai ya kumtetea mwanae ambaye alipata maficho katika boma hilo. 

.
RELATED VIDEOS