23rd March, 2022
Dereva wa madktari wawili wa Cuba waliotekwa nyara katika kaunti ya Mandera na kupelekwa nchini Somalia mwaka 2019 amehukumiwa kifungo cha maisha jela. Issack Ibrein Robow atahudumia kifungo hicho cha maisha kwa kufanya kitendo cha kusaidia ugaidi kilichosababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi. Hakimu mkuu Martha Nanzushi pia alimuadhibu kifungo cha miaka 40 na miezi sita jela kwa makosa mengine matatu.