23rd September, 2020
Gavana wa Machakos Alfred Mutua amemtaka kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kukoma kuiga mikakati yake ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022. Mutua aliyezungumza huko Machakos amemtaka Mudavadi kuwa mbunifu anaponadi ajenda zake, akidai kwamba kupitia uongozi wa chama chake cha Maendeleo chap?chap, yeye ndiye sura mpya kwenye kinyang'anyiro hicho cha urais na ndiposa Mudavadi anajaribu kumuiga