.
18th September, 2020
Huku siasa zikiwa zimechacha nchini baadhi ya viongozi wa kaunti ya west pokot sasa wamekashifu siasa wanazosema zinanuiya kugawanya taifa wakisema zitarejesha nyuma maendeleo kwenye kaunti. Aidha viongozi hao waliokuwa wakizungumza kwenye maadhimisho ya miaka mitatu ya uongozi wa gavana wa kaunti hiyo john lonyangapuo walichukua fursa hiyo kumtetea kufuatia tishio kwamba huenda akatimuliwa kutoka chama cha kanu.