16th September, 2020
Wakaazi wa Kaunti ya Mandera wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji huku wakilazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta bidhaa hiyo muhimu. Wakazi hao sasa wanalalamikia hatua ya serikali ya kaunti kulifumbia macho tatizo hilo wanalosema limewahangaisha kwa muda sasa.