16th September, 2020
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ataendelea kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Central mjini Nakuru hadi Jumatano wiki ijayo ili kuuwezesha upande wa mashtaka kumaliza uchunguzi. Hakimu Mkuu Josephat Kalo alisema kuwa Korti ilikuwa imeridhishwa na ombi la upande wa mashtaka lakini badala ya siku kumi na nne waliotaka, wakapata siku saba.