.
3rd June, 2020
Viongozi wa utawala na wa kisiasa katika eneo la njoro kaunti ya nakuru, wameafikiana kuhakikisha amani inadumu katika kijiji cha bondeni katika eneo hilo. Majuma mawili yaliyopita,mzee wa makamo aliuawa kinyama hatua iliyochochea makabiliano baina ya jamii zilizoko eneo hilo. hatahiyvo, wakazi na viongozi wa kisiasa wamewanyooshea maafisa wa usalama kidole cha lawama kwa kile wanachokitaja utepetevu kazini.