25th March, 2019
Mfanyabiashara mmoja maarufu jijini mombasa amefikishwa mahakamani baada ya kukamatwa siku ya jumamosi akiwa na kilo moja ya dawa aina ya heroin yenye thamani ya shilingi milioni 1.5. Abdul majid msallam timami aliye na umri wa miaka 47 amefikishwa katika mahakama ya mombasa leo ambapo amesomewa mashtaka dhidi yake.
Kulingana na idara ya upelelezi, dci dawa hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya mfuko na zilikuwa zikisafirishwa kwa gari aina ya honda.timami anashtumiwa kuwatumia vijana kuziuza dawa hizo, hali ambayo imesababisha wengi wao kukosa kwenda shuleni na badala yake kujiingiza katika biashara haramu ya ulanguzi wa dawa za kulevya.aidha ameshtumiwa kumiliki malori makubwa makubwa katika ukanda wa afrika mashariki huku akiyatumia katika biashara haramu.inaarifiwa amekuwa akiendesha biashara hiyo kwa kipindi cha mwongo mmoja katika eneo la tudor kaunti ya mombasa.mahakama imemwachilia kwa dhamana ya shilingi millioni moja.kesi hiyo itaskizwa aprili 14.