.
3rd September, 2018
Waendeshaji magari pamoja na wasafiri wa magari ya umma kote nchini wanaendelea kulalamikia nyongeza ya bei ya mafuta iliyosababishwa na ongezeko la ushuru wa asilimia kumi na sita wa bidhaa za mafuta. Hii leo baadhi ya waendeshaji magari walifanya maandamano mjini nakuru wakishinikiza serikali kubatilisha uamuzi huo wakisema nyongeza ya bidhaa za mafuta itafanya gharama ya maisha kupanda zaidi. Mwanahabari wetu elphas lagat kutoka nakuru alifuatilia maandamano hayo.