3rd September, 2018
Zaidi ya viongozi 50 wa mataifa ya Bara Afrika wako mjini Beijing nchini Uchina kushiriki katika kongamano la siku mbili la ushirikiano kati ya mataifa ya afrika na uchina. Kongamano hili linajiri wakati mataifa mengi ya afrika yamekosolewa kutokana na mzigo wa madeni ambayo yamejitwika kutoka uchina. Kongamano hilo ambalo hufanyika kila baada ya miaka mitatu hutoa fursa kwa uchina kunadi mikopo kwa mataifa ya afrika. Kongamano hilo lilianza kwa mkutano baina ya rais xi jinping na viongozi hao wa afrika.