3rd September, 2018
Kilio cha kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli sasa kiko vinywani mwa Wabunge wa mirengo yote ya kisiasa. Mwakilishi wa kike wa Kaunti ya Nyandarua Faith Gitau amemsuta waziri wa fedha henry rotich kwa kuwapuuza wabunge na kuendeleza kutekeleza nyongeza ya ushuru wa ziada kwa bidhaa za mafuta ya petroli. Aidha faith ametoa wito kwa serikali kupandisha misharaha ya wafanyikazi wa umma ili waweze kuyamudu maisha ambayo gharama yake ya juu imembana koo kila mkenya.