Vyongozi wa chama cha KANU wadokeza kuwa huenda KANU ikawania urais katika uchaguzi ujao
8th May, 2016
Viongozi wa chama cha KANU wakiongozwa na mwenyekiti Gideon Moi wamedokeza kuwa huenda KANU ikawania urais katika uchaguzi ujao. Aidha viongozi hao walisema kuwa chama cha Jubilee kimekuwa kikiitumia jamii ya wakalenjin kwa manufaa ya watu binafsi. Kadhalika wamesema kwamba hawaoni sababu ya kusubiri hadi mwaka 2022 kama Naibu Rais William Ruto anavyowataka watu kufanya. Viongozi wengine waliozungumza ni pamoja na maseneta john lonyangapuo na zipporah kittony waliosistiza kuwa kamwe hawatakivunjilia mbali chama cha KANU .