Gavana Kidero afika katika eneo ya mafuriko eneo wa Huruma
1st May, 2016
Gavana wa Nairobi Evans Kidero hatimaye amezuru eneo la mkasa wa kuporomoka kwa jengo la makazi huko Huruma, jijini Nairobi. Kidero amesema Kaunti ya Nairobi imetenga fedha za kuwasaidia waathiriwa. Aidha Gavana Kidero amelaumu mwingilio wa kisiasa katika maafa ya majumba kuporomoka akiahidi kwamba kufikia jumatano ijayo, hatua zitachukuliwa dhidi ya walioidhinisha jumba hilo lisalie wima licha ya kutofaa kwa makazi. Mvua inaendelea kunyesha, huku shughuli zauokoaji zikiendelea nayo idadi ya waliofariki ikizidi kupanda kutoka kumi hapo jana hadi kumi na sita asubuhi ya leo. Wasiojulikana waliko nao ni 69 kufikia sasa huku manusura wakiwa 134.