CORD yakashifu Serikali ya Jubilee huko kiwanja ya Kamukunji
23rd April, 2016
Muungano wa upinzani nchini CORD, ulifanya mkutano wake hii leo katika uwanja wa Kamkunji na kukashifu serikali ya Jubilee kuhusu ufisadi uliokithiri nchini. Wakuu wa CORD wakiongozwa na Raila Odinga, Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka wamezungumzia masuala ya Eurobond na vilevile kutaka serikali ihakikishe kuwa kuna utangamano miongoni mwa wananchi kabla ya uchaguzi mkuu ujao.