Wabunge wataka wanafunzi 5,101 waliokosa matokeo yao ya mtihani kupewa matokeo yao
29th March, 2016
Siku moja kabla kuanza kongamano la kujadilia mfumo wa elimu nchini, kukiwemo mapendekezo ya kuubadilisha, kamati ya bunge kuhusu elimu imekutana na waziri wa elimu Dkt. Fred Matiangi kupokea ripoti maalum kuhusu uozo katika baraza la taifa la mitihani. Aidha wabunge wametaka wanafunzi 5,101 waliokosa matokeo yao katika mtihani wa mwaka jana kupata matokeo hayo wakisema makosa yalitokana na utepetevu wa baraza la knec wala si wao.