KTN Leo kamilifu 10 Machi 2016 - Ndegwa Muhoro yu matatani
10th March, 2016
Wakili Ahmednassir Abdullahi sasa anataka hatua za dharura kuchukuliwa dhidi ya mkurugenzi mkuu wa idara ya CID Ndegwa Muhoro kwa madai ya kuhusika na hongo ya shilingi milioni hamsini kubatilisha kesi ya Tatu City. Kando na hayo wakili Ahmednassir amemtaka mkuu wa polisi kuanzisha uchunguzi dhidi ya afisa mkuu wa cid kwa kuongoza mitandao ya wafisadi.