Rubani wa naibu wa rais William Ruto Alastair Lleweyln atiwa mbaroni kwa kumpiga afisa wa polisi
23rd February, 2016
Rubani wa ndege iliyombeba naibu wa rais William Ruto Alastair Lleweyln hatimaye anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimani baada ya hisia kali kutoka kwa wakenya waliomkashifu kwa kumchapa afisa wa polisi katika kaunti ya nyandarua. Mapema leo naibu rais ametoa wito kwa polisi kumtia nguvuni kufuatia hamasa ya wakenya kwenye mtandao