Simba mmoja apatikana na maafisa wa KWS huko Lang’ata
20th February, 2016
Maafisa wa shirika la huduma kwa wanyama pori KWS, wamefanikiwa kumwona simba mmoja kati ya wale walioripotiwa kutoweka. Simba huyo jike alionekana ijumaa jioni kwenye msako maeneo karibu na kambi ya kijeshi ya Lang’ata.