KTN Leo Kamilifu Sehemu ya Kwanza Februari 19,2016
19th February, 2016
Taharuki imetanda maeneo ya Lang’ata, Kibra na eneo zima la Southern Bypass jijini Nairobi baada ya simba kuripotiwa kutoka nje ya mbuga ya kitaifa ya Nairobi. Kwa mujibu wa maafisa wa shirika la wanyama pori KWS, simba hao takriban sita, walianza kuelekea eneo la kijeshi la Langa’ta Barracks kando na mbuga hiyo na baadaye wakatoweka. Raia wameombwa kuwa macho na kuripoti simba watakaowaona huku msako wa kws ukiendelea.