Muuguzi aliyeaga dunia kutokana na Ebola azikwa kwao Luanda
16th January, 2016
Edith Dorothy Ong’ondo,mmoja wa wauguzi waliojitolea kukabiliana na janga la Ebola nchini Sierra Leone hatimaye amezikwa huko Luanda katika kaunti ya Vihiga. Familia yake inadai kuwa Edith, aliyeanza kuugua maradhi ya utandu wa ubongo yaani meningitis nchini Sierra Leone, asingalitaabika kiasi cha kufa iwapo angalitunzwa ipasuavyo aliporejeshwa nchini.