Unyama: Mwanamume mwenye umri wa miaka 42 ambaka bintiye Murang’a
3rd January, 2016
Kwenye kisa kinachoibua maswali kuhusu uhusiano wa wazazi wa kiume na mabinti zao, mwanamume mmoja katika kaunti ya Murang’a ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumbaka bintiye. Patrick Ng’ang’a mwenye miaka 42 anadaiwa kumtendea mwanawe wa darasa la tano unyama huo wakati mkewe alipoondoka kujumuika na jamaa zake kwa sherehe za mwaka mpya.