Wakenya wabuni njia za kuwatafuta jamaa zao wanaopotea kupitia mtandao
3rd January, 2016
Visa vya Wakenya kupotea au kuwapoteza wapendwa wao kwa njia ya kutatanisha vimeongezeka. Na sasa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa utepetevu wa idara za usalama, Wakenya wengi wamebuni njia za kuwatafuta jamaa zao mojawapo ikiwa ni kupitia mtandao. Francis Mtalaki alikutana na Christine Kagendo ambaye tangu septemba mwaka jana amekuwa akimtafuta mwanawe bila mafanikio.