Licha ya Kenya kuwa na bahari, Kenya huagiza samaki kutoka Uchina
26th December, 2015
Licha ya Kenya kuwa na bahari yenye urefu wa takriban kilomita 700, yenye uwezo wa kuzalisha samaki, Kenya inaagiza samaki kutoka Uchina kuuzwa katika soko humu nchini. Ni kauli iliotolewa na waziri anaehusika na maswala ya uvuvi na kilimo kaunti ya Mombasa Anthony Jaramba, ambaye anasisitiza uhaba wa vifaa umepelekea wavuvi wengi kukata tama na shughuli za uvuvi ukanda wa pwani. Nilipata fursa ya kuzuru mojawapo ya bandari kuu ya samaki inayotumiwa kaunti ya Mombasa,na kukuandalia taarifa inayoangazia changamoto za sekta uvuvi sehemu hio.