Timu ya Soka ya Utawala wachukua ubingwa wa Mureithi Cup
14th December, 2015
Kombe la Mureithi kiliingia tamati hapo jana ambapo utawala walichukua ushindi baada ya Kuwafunga Dallas fc mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti. Mashindano hayo ambayo yalitazamiwa kuwapa nafasi vijana hasa wale wanaotoka vitongoji duni kuonyesha ueledi wao yalivutia mamia ya mashabiki wakiwemo naibu mkufunzi wa harambee stars musa otieno na mahmud abbas.