Makala ya 13 ya mbio za Standard Chartered yapangwa kufanyika siku ya Jumapili
22nd October, 2015
Makala ya 13 ya mbio za Standard Chartered yatakayofanyika siku ya jumapili yanatarajiwa kuvutia watu wengi. Wasimamizi pamoja na idara ya Polisi wanafanya matayarisho ya mwisho kuhakikisha kila kitu kitaenda shwari huku wakidokeza kuwa baadhi ya barabara zitafungwa jambo ambalo litaathiri wasafiri.