Bodi ya uchaguzi wa FKF yalaumiwa kwa kutomakinika
14th October, 2015
Huku zikiwa imesalia siku chache kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi wa shirikisho la kandanda nchini, bodi ya uchaguzi wa FKF inanyoshewa vidole vya lawama na baadhi ya washika dau wa soka nchini kwa kile kinacho tajwa kama kutomakinika. Kulingana na Doris Petra ambaye ni naibu wa mgombeaji Nick Mwendwa pamoja na David Gikaria mwenyekiti wa tawi la eneo la Central Rift, bodi ya uchaguzi chini ya uongozi wa Donald Kipkorir haijaandaa mkutano hata mmoja, jambo litakalo lemaza uchaguzi ujao.