Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na Zipora Kering wamtetea Ann Waiguru
5th October, 2015
Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen pamoja na Zipora Kering wameikosoa hatua ya kumtaka waziri wa ugatuzi Ann Waiguru kujiuzulu ama kubanduliwa uongozini kwa madai ya ufisadi katika afisi ya huduma kwa Vijana Wa Taifa NYS. Katika kauli zilizoonekana kumpinga mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter anayeisukuma Agenda ya kumbandua Waiguru, Murkomen amesema kwamba mawaziri waliotupwa nje kwa madai ya ufisadi warudishwe afisini iwapo swala ni kwamba orodha ya tume ya kupambana na ufisadi EACC ilikuwa na dosari.