Mahujaji sita kutoka Kenya wathibishwa kufariki wakati wa ibada ya Hajj nchini Saudia
29th September, 2015
Mahujaji sita kutoka humu nchini wamethibishwa kufariki wakati wa ibada ya Hajj, huku wengine tisa wakiwa hawajulikani walipo. Wakitoa takwimu hizi baraza kuu la waislamu nchini Supkem, limeongeza kuwa litatoa ripoti yake kuhusiana na vifo vya mahujaji nchini Saudia punde tu wasimamizi wake wa hajj watakaporejea humu nchini.